• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
MADABA DISTRICT COUNCIL
MADABA DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Madaba

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Department and Section
  • Investment
  • Huduma
    • Huduma ya Kwanza
    • Huduma ya Pili
  • Councillors
  • Miradi
    • Mradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa
    • Matukio
  • Divisheni

DED Madaba atoa maagizo kwa watumishi

Posted on: May 17th, 2024

MKURUGENZI Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Madaba Sajidu Idrisa Mohamed amewaagiza watumishi wa Hospitali ya Wilaya kuwepo eneo la kazi na watumishi waliopewa nyumba katika eneo la Hospital kuhamia mara moja.

Hayo amesema alipotembelea hospitali hiyo na kukagua vifaa tiba vilivyoletwa na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan na ujenzi wa wodi za wanaume,wanawake,watoto,jengo la wazazi na jengo la dharula.

“Mmeletwa hapa kwaajili ya kutoa huduma kwa wananchi hospitali imeanza kutoa huduma na vifaa tiba vyote vipo nyumba za watumishi zipo  watumishi mliopewa nyumba hamieni haraka iwezekanavyo “.

Hata hivyo amemwagiza mhandisi wa Halmashauri hiyo kuhakikisha anakamilisha marekebisho  yote ambayo yapo katika ujenzi wa hospitali hiyo awe amekamilisha na amemwgiza mganga mkuu wa Halmashauri kuweka kibao kinachoelekeza Hospitali ilipo baada ya wiki moja wawe wamekamilisha.

Pia Mkurugenzi amewaagiza watumishi wote wanaotakiwa kuhamia hospitali ya Wilaya kuhama katika ofisi ya Mkurugenzi haraka iwezekanavyo akiwemo katibu wa Afya ,Afisa ustawi wa jamii,Afisa Lishe wahakikishe wanatolea huduma katika hospitali ya Wilaya.

“Wote wenye ofisi katika hospitali ya Wilaya wahame sitaki kuwaona katika jengo la halmashauri Afisa utumishi waandikie barua ya kuwany’ang’anya vyumba vyao na wahamishe vitu vyao hayo ni maelekezo yangu”.

Kutoka kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Madaba

Mei 16,2024

Matangazo

  • VIGEZO vya kupata Lesen May 17, 2022
  • Angalia zote

Matangazo Mapya

  • Uboreshaji wa Daftari la kudumu jimbo la Madaba

    January 20, 2025
  • Jitokeze kujiandikisha

    January 20, 2025
  • Chwaya atoa rai kwa walimu wa awali kutekeleza agizo la Serikali

    January 18, 2025
  • MARATIBU wa mradi wa BOOST Madaba amshukuru Rais Samia

    January 18, 2025
  • Angalia zote

Video

WADAU WATOA MAONI JUU YA MAADILI KWA VIJANA
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Ruvuma-webportal
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Nyasa District Council
  • Ega Website
  • Namtumbo District Council
  • Mbinga Town Cuncil
  • Songea District Council
  • Songea Municipal Council

Kurasa Mashuhuru

  • NECTA
  • Tanzania Revenue Authority
  • Tanzania Forest Agency
  • Watumishi portal
  • Livestock Training Agency (LITA) Madaba
  • Parliament

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana Nasi

    MADABA - RUVUMA

    Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA

    Simu: 0252951052

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: ded@madabadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Falagha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya Mahali
    • Huduma

Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa