MWENGE wa Uhuru katika Halmashauri ya Madaba umezindua Kikundi cha Maarifa Mtyangimbole kinachojishughulisha na Ujasiliamali.
Mwenyekiti wa Kikundi hicho Annamaria Komba akisoma taarifa kwa kiongozo wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Sahil N. Geraruma amesema kikundi hicho cha wanawake kilianzishwa mwaka 2019 na kusajiliwa mwaka 2021 kwa hati na RVM/MADDC/20210810095919467 kikiwa na wanachama wanawake 10.
Mwenyekiti ameelezea lengo la kikundi hicho ikiwa nipamoja na kuleta umoja na Mshikamano pamoja na kuinuana Kiuchumi kupitia ujasiliamali mdogo mdogo kwa kutengeneza sabuni,batiki,vitafunwa na unga wa Lishe.
Amesema kikundi hicho kilianza shughuli za utengenezaji wa sabuni za maji na vipande kwa mtaji wa shilingi elfu tisini kwa kununua malighafi na vifungashio na kupata faida ya shilingi elfu sitini.
Komba amesema uzalishaji wa bidhaa mbalimbali zinazozalishwa na faida iliyokuwa ikipatikana walihifadhi katika kibubu hadi kufikia Desemba 30, 2021 kikundi kilikuwa na zaidi ya shilingi milioni moja na kutokana na faida hiyo kikundi kiliongeza uwigo wa biashara na kuomba mkopo Halmashauri.
Hata hivyo amesema Kikundi kilipata Mkopo wa Milioni kumi kutoka Halmashauri ya Madaba na kununua vifaa mblimbali ikiwemo mashine 2 za kusaga malighafi,pamoja na malighafi za kutengenezea biashara mbalimbali.
“Mkopo umetusaidia kupata mafanikio mblimbali ikiwemo kuongeza uzalishaji,kufungua account,kupata jiko la kisasa kwaajili ya kuoka vyakula na kuhakikisha mwanakikundi anainuka kiuchumi”.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mara baada ya taarifa hiyo amempongeza Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo kwa kusimamia zoezi la Mikopo inayotolewa na Halmashauri kwa kuhakikisha wanakikundi wanarejesha kwa wakati.
Kiongozi huyo amewaagiza wakurugenzi wa Halmashauri na Manispaa kuhakikisha mikopo yote inayotolewa irejeshwa kwa wakati ili na vikundi vingine viweze kupata mikopo hiyo.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma
Aprili 15,2022
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa