KAMATI ya ushauri Wilaya ya Songea (DCC) imeridhia ongezeko la maeneo Mapya ya Yerusalaem na Tunduma kuwa sehemu ya shamba la Miti lililopo Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.
Mkuu wa Wilaya ya Songea Kapenjama Ndile akizungumza katika Kikao hicho amesema wananchi wanaoishi katika maeneo hayo wapewe fidia ili waweze kuhama katika eneo hilo na kuweza kuongeza maeneo mapya ya shamba la miti.
Afisa misitu wa Shamba hilo Mustafa Yange akisoma taarifa kwaniaba ya Muhifadhi Mkuu wa Shamba la Miti Wino Grory Fotunatus amesema kijiji cha Wino kilitoa ardhi hekta 2,038.955 kwaajiji cha upandaji wa miti.
Hata hivyo amesema walifanya mkutano wa Kijiji uliofanyika Oktoba 27,2012 kuwa wananchi wa eneo hilo walikubaliana na TFS Wino kuongezewa eneo la hekta 2000 kwa masharti kuwa eneo jipya litatolewa baada ya wakala wa Misitu kumaliza kupanda eneo la awali.
“Tunaomba Serikali kutufikilia na kutupatia eneo hususani upande wa tunduma Wino,kitongoji cha Yerusalem kilichopo Magingo Kata ya Mkongotema tubadilishe matumizi kwa lengo la kuongeza uhifadhi na kupunguza Majanga “.
Yange ametoa sababu ya kuhifadhi eneo hilo ili kuepuka kuhatarisha ustawi wa uhifadhi ya misitu ya tarafa ya Ifinga na Mkongotema kuchoma Moto hovyo unaofanywa kila mwaka na kusababisha hasara na kuunguza hekari nyingi za Misitu ya TFS na Wananchi.
Amesema eneo linapitiwa na mto Lutukila na Lupahila unaopeleka maji bonde la Ziwa Nyasa ikiwa wakazi wa kitongoji hicho wanalima na kuchoma moto hadi kingo za mto pamoja na uwindaji haramu wa wanayama pori.
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
Januari 19,2024.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa