MKUU wa Wilaya ya Songea Wilman Ndile amewaagiza watendaji wa vijiji na Kata kuhakikisha wanafunzi wa kidato cha kwanza wanaripoti shuleni.
Hayo amesema alipoongea na watumishi wa Halmashauri ya Madaba katika ukumbi wa Halmashauri ikiwa ni siku ya tatu tangu kuanza kazi mara baada ya kuapishwa.
Amesema watendaji wa vijiji walichukulie hili swala kwa uzito kama kuna mwaka hawajawahi kufikia asilimia ya wanafunzi kujiunga na kidato cha kwanza mwaka huu wahakikishe wanafikia asilimia hizo.
“Nitaweza kuelewa tu wale ambao wamekwenda seminari, shule nyingine binafsi, amefariki na tunataarifa zao la sivyo watafutwe popote ”.
Mkuu wa Idara ya Elimu Sekondari Maternus Ndumbaro wa Halmashauri hiyo amesema mpaka kufikia Februari 2 wanafunzi wa kidato cha kwanza walio ripoti shuleni wamefikia asilimia 89.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa