HALMASHAURI ya Madaba wamefanya kikao cha Baraza la Madiwani cha robo ya mwaka kuanzia Julai 2022 hadi Septemba 2022.
Akizungumza Mkuu wa Wilaya ya Songea Pololeth Mgema katika Baraza hilo lililofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ameagiza kuhakikisha miradi mipya ya ujenzi wa Madarasa 10 katika Halmashauri hiyo ifikapo Desemba 10,2022 iweimekamilika.
Mgema amesema atafanya ziara ya ukaguzi kwaajili ya kuangalia ukamilifu wa Madarasa pamoja na thamani ya fedha na kiwango cha ubora wa ujenzi wa miradi hiyo.
“Sina mashaka juu ya muda tulijiwekea tarehe hiyo kwasababu tunataka tukamilishe ili tuendelee na mambo mengine na madarasa hayo kwaajili ya kidato cha kwanza mpaka kufikia Januari madarasa yatakuwa yamekamilika”.
Hata hivyo Mkuu wa Wilaya ameelekeza kuhakikisha miradi ya Mda mrefu ikiwemo Hospital ya Wilaya inayojengwa kwa zaidi ya shilingi bilioni 2 kukamilika pamoja na mradi wa nyumba tano za watumishi ifikapo mwaka mpya 2023.
Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Teofanes Mlelwa akifunga kikao hicho cha Baraza amewasisitiza Madiwani kuhakikisha wanasimamia miradi pamoja na ukusanyaji wa Mapato katika Kata zao.
Amesema ifikapo Januari 1,2023 kufuatia tarehe hiyo kuwa siku ya kupanda miti kitaifa ametoa rai kwa Mkurugenzi kutafuta eneo la kupanda miti pamoja na maeneo mbalimbali na Watendaji kata kusimamia katika maeneo yao.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka kaitengo cha Mawasiliano Serikalini Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Madaba
Desemba 6,2022.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa