MKUU wa Wilaya ya Songea Pololeth Mgema amechangia mifuko 40 Saruji yenye thamani ya Shilingi 680,000/= katika shule ya Sekondari Lilondo iliyopo kata ya Wino Halmashauri ya Madaba.
Akizungumza mara baada ya kukagua shule hiyo na kuendelea na zoezi la upandaji miti katika eneo la Shule hiyo amesema Kata ya Wino wameona umuhimu wa kuwa na Shule nyingine ambayo itasaidia kupunguza msongamamno wa wanafunzi katika Shule ya Wino.
“Wanalilondo mmeona Shule ya Sekondari Wino haitoshi ndipo mkaanzisha Shule ya Sekondari ili kuhakikisha wanafunzi wanasoma kwa raha nimekuja hapa kabla ya zoezi la upandaji wa miti nimeona juhudi zenu hongereni sana”.
Mgema ametoa wito kwa wananchi wote kuhakikisha wanawaandikisha watoto kuanzia miaka 4 darasa la awali mpaka darasa la kwanza ifikapo Januari 9,2023 wawepo darasani masomo.
“Darasa la awali na Darasa la kwanza Januari 9 wawepo darasani katika hilo serikali haitafanya mchezo kuchukua hatua”.
Hata hivyo amesema Rais wa Jamhuri za Muungano wa Tanzania amesema Elimu itatolewa bure kuanzia Darasa la awali hadi kidato cha zaidi ya mzazi kuhakikisha wanapewa mahitaji yote muhimu.
Mkuu wa Wilaya amesisitiza kuhakikisha wazazi wanachangia chakula cha mwanafunzi awapo Shuleni ili kuhakikisha wanajisomea vizuri na kustawi kiafya na kiakili.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Halmashauri ya Madaba
Januari mosi,2023.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa