MKUU wa Wilaya ya Songea Wilman Ndile amewataka watendaji Kata na Vijiji kutoa takwimu sahihi kwa upande wa afua za Lishe .
Hayo amesema alipofunga Kikao cha tathimini ya utekeleza wa Mkataba wa Lishe robo ya kwanza mwaka 2023/2024 katika Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.
“Muwahimize wale waliopo chini yenu wawaletee takwimu sahihi ,tukiwa na takwizmu zisizo sahihi kwa maswala ya Lishe mnaivuruga jamii”
Ndile amewaeleza watendaji kuwahimiza watoa huduma wa ngazi ya vijiji kutoa takwimu sahihi katika Kaya,Kijiji, Kata hadi Halmashauri.
Hata hivyo ametoa rai kwa watendaji hao kusimamia sheria ndogo kwa wazazi wanaosuasua utoaji wa chakula mashuleni ikiwa wanasababisha watoto wasifanye vizuri katika masomo yao.
“Ninyi watendaji kwa mamlaka mliyopewa muwahimize wazazi na kuwabana ambao hawatoi chakula shuleni”
Ndile amesema wahakikishe wanawatembelea watoa huduma ngazi ya vijiji na kuwatia moyo iliwaweze kufanya kazi ya usimamizi wa Lishe kwa bidii.
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
Oktoba 25,2023.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa