Mkuu wa Wilaya ya Songea Kapenjama Ndile amewapongeza wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Madaba kwa kutambua umuhimu wa kutunza Misitu.
Ndile ameyasema hayo alipomwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Ahmed Abbas Ahmed katika zoezi la uzinduzi wa upandaji Miti amesema mwaka 2024 wananchi wamekuwa waungwana kwa kuacha kuchoma moto hovyo katika misitu.
“Wananchi mme kuwa watu wema mmelinda msitu wa Serikali na mmekuwa waungwana mmejifunza mnabadilika mmetambua umuhimu wa misitu katika Wilaya yetu na miche 200,000 mmepewa bure na Serikali kupitia Ofisi ya uhifadhi Wino (TFS).
Amesema adui mkubwa wa misitu ni moto na TFS wamegundua teknolojia mpya ya kutambua mtu aliyeanzisha moto ili aweze kukamatwa nakupewa adhabu.
Hata hivyo amesema katika Nchi ya Tanzania uchumi unaoongoza ni wakijani wa upandaji miti na miti ya asili.
“Madaba tunabahati tunamisitu ya kupanda na asili nataka niwaambie Wilaya zote ambazo wamewekeza katika miti ya kupanda umaskini umekuwa historia kwa mfano Mufindi”.
Kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
Januari 7,2025.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa