MKUU wa Wilaya ya Songea Wilman Ndile amefanya kikao kazi cha kujua hali ya Elimu katika Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.
Kikao hicho kimefanyika katika Shule ya Sekondari ya Joseph Mhagama kilichojumuisha wataalam ngazi ya Halmshauri Walimu wakuu,Maafisa Elimu Kata,Watendaji wa Vijiji na Kata.
Ndile akizungumza katika Kikao hicho amewaagiza Maafisa Elimu Kata, watendaji kata na vijiji kuhakikisha ifikapo Februari 3,2024 wanafunzi wa kidato cha kwanza waliopangiwa kuripo shuleni Mwaka huu 2024 wawe wameripoti kwa asilimia 99.
‘Mimi Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi,watendaji kata na vijiji,Maafisa Elimu Kata tuhakikishe kila mwanafunzi aliyechaguliwa kujiunga kidato cha kwanza,darasa la awali na darasa lakwanza tuhakikishe wanaripoti labda kama ameenda shule binafsi nimewaiteni hapa kuwapa maelekezo haya kwa msisitizo mkubwa”.
Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji wa Halmshauri hiyo Sajidu Idrisa Mohamed amesema kupitia maelekezo aliyotoa Mkuu wa Wilaya amemwakikishia kabla ya Mwezi Februari 2024 watakuwa wamefikia asilimia 100.
“Nikuhakikishie Mkuu wa Wilaya kabla ya Mwezi Februari tutakuwa tumefikia zaidi ya asilimia 100 kwa lengo la madarasa yaliyojengwa yaweze kupata wanafunzi ikiwa wanaoendelea kuripoti kila siku”.
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Madaba
Januari 17,2024.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa