Kufuatia zao la ufuta kuzwa kilo shilingi 3,800/= Mkuu wa Wilya ya Songea Wilman Ndile amewasisitiza wananchi wa Halmashauri ya Madaba kulima zao hilo.
Hayo amesema baada ya kikao kazi cha Elimu kilichofanyika katika Shule ya Joseph Mhagama ikiwa mwaka 2023 Halmashauri ya Madaba wamekusanya ushuru kupitia zao la ufuta zaidi ya shilling Milioni 10.
“Ni vizuri tukaweka mkazo kwenye zao la ufuta Halmashauri ya Namtumbo sehemu kubwa ya mapato yao yametokana na ufuta,tumbaku na mahindi na Halmashauri ya Kilwa Ruangwa,Nachingwea asilimia ya mapato yake yalitokana na ufuta”.
Hata hivyo amesema kama viongozi wajibu wetu ni kuwapa wananchi matumaini ikiwa Halmashauri ya Madaba zao hilo linastawi vizuri .
“Mkuu wa Idara ya Kilimo ahakikishe anatafuta mbegu kwaajili ya wananchi na mimi mkuu wa Wilaya nitajitaidi kutafuta mbegu “.
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Madaba
Januari 17,2024.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa