WAZAZI na walezi wameaswa kulea watoto katika maadili mazuri na kuwapangia mikakati ambayo itawawezesha kutimiza ndoto zao.
Hayo amezungumza afisa wa porisi dawati la jinsia Halmashauri ya Wilaya ya Madaba Antony Mtokambali katika maadhimisho ya siku ya wajane yaliyofanyika Juni 27,2024.
Hata hivyo amesema katika jamii kumekuwa na ukatili wa kijinsia kwa watoto ambao unaweza kupelekea kutotimiza ndoto zao na kupunguza nguvu kazi ya Taifa.
“kuna aina tatu za ukatili wa kimwili,kingono na kisaikolojia kulingana na vitendo hivi vya ukatili toa taarifa ili tuweze kuwashughulikia watu wanaofanya ukatili ,hatukatai watoto wanafanya makosa mbalimbali aadhibiwe kidogo ndiomana tunatoa elimu”.
Aidha Mtokambali amesema ukatili wa kingono unawe kuleta athali kwa watoto kama kuambukizwa magonjwa mbalimbali na kuasababisha kifo.
“Sisi na nyie wazazi tukiungana na kupata taarifa sahihi tunaweza kudhibiti vitendo vya ukatili sasahivi kuna wimbi kubwa sana watoto wadogo wanafanyiwa ukatili”.
Kutoka kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
Juni 27,2024.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa