Katibu Tawala Wilaya ya Songea Mtela Mwampamba ametoa rai kwa waheshimiwa Madiwani na wataalam kuhakikisha miradi ya Maendeleo ambayo inaletwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inasimamiwa na kukamilika kwa wakati.
Akitoa salamu katika mkutano maalum wa baraza la madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Madaba amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ameleta zaidi ya shilingi bilioni tatu kwaajili ya ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ambayo imeanza kutoa huduma.
“Pamoja na kutujengea miundombinu na kuleta vifaa tiba mbalimbali ametuletea watumishi 150 wakiwa 74 ni watumishi wa afya “
Hata hivyo amewaomba wananchi wa halmashauri hiyo kujenga nyumba ambazo zitawasaidia watumishi hao kupanga ili waweze kupata mazingira mazuri ya kuishi.
“Tumeanza kujenga nyumba za watumishi lakini hatuwezi kujenga kwa watumishi wote rai yangu baada ya kuwekeza kwenye kilimo tu tuwekeze na kwenye ujenzi wa nyumba ardhi ni bei ya chini umeme upo lakini nyumba hazipo”.
Hata hivyo amelaani vikali baadhi ya mabaraza ya ardhi ya kata kutoa hukumu ya migogoro ya ardhi badala yake watoe suluhishi.
“Ukiangalia ni kinyume cha sheria kifungu cha 13 na 3 cha maboresho ya sheria ya mwaka 2021 kinakataa mabaraza ya ardhi ya kata kutoa hukumu Madiwani na wananchi wote wajue juu ya utatuzi wa mabaraza ya ardhi”.
Imeanadaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka akaitengo caha Mawasiliano Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
Agosti 27,2024.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa