Katibu Tawala Wilaya ya Songea Mtela Mwapamba amewaagiza watendaji Kata na vijiji kutokuruhusu taasisis yoyote ya kidini kufanya shughuli bila kusajiliwa na Wizara ya mambo ya ndani.
Mwampamba akitoa salam katika baraza la amadiwani la kufunga mwaka katika halmashauri ya Wilaya ya Madaba amesema kuna baadhi ya taasisi hizo zipo kwaajili ya kuharibu uchaguzi wa Serikali za mitaa na uchaguzi mkuu ili Nchi ya Tanzania ionekane inataswira mbaya.
Hata hivyo Mwapamba ameiagiza halmashauri hiyo kudhibiti mianya ya upotevu wa mapato ya ndani na kudhibiti ongezeko la madeni mapya.
“Hatuwezi kuendesha Halmashauri bila makusanyo Nimepita katika kituo cha kukusanya mapato Likarangiro nimeona mapato yanapotea na mizigo ya mkaa inapitishwa,pia naomba tupunguze ongezeko la madeni mwakajana hamashauri ilikuwa na madeni mengi sana”.
Aidha Mwampamba amesema tangazo la Serikali za mitaa limesha tangazwa kuwa viongozi wote walio katika ngazi ya msingi za vijiji waweze kupata tangazo hili kwa maandishi.
“Tunajua itakapofika Oktoba 25,2024 inatakiwa ndugu zetu viongozi kutoka ngazi ya kijiji wanatakiwa kuondoka katika madaraka yao naomba wapate taarifa hii kwa maandishi ili wasifanye mambo tofauti na serilaki ”.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa