Katibu Tawala Wilaya ya Songea Mtela Mwampamba ameipongeza benki ya NMB kwa kuunga mkono jitihada za Rais Samia katika kuendeleza maendeleo ya sekta za Afya na elimu.
Hayo amesema katika hafla fupi ya kukabidhi vifaa vya na elimu katika halmashauri ya Wilaya ya Madaba na benki ya NMB ambayo wametoa vitanda,magodoro,madawati vilivyogharimu kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 49.
“NMB ni benki ambayo inatupa sapoti sana sisi Watanzania kwa kurudisha faida kwa jamii inayopatikana, wamefanya hivyo ikiwa watu wa Madaba tunawaunga mkono”.
Hata hivyo Mwampamba amewakumbusha wananchi kwa kipindi hiki cha kuanadaa mashamba wahakikishe wanalinda mazingira na kuepuka uchomaji wa moto holela.
“Tumepata hasara sana tukichoma moto tunaharibu guzo za umeme zinaungua na kusababisha umeme kukatika mara kwa mara ,mashamba ya miti kuungua ikiwa Serikali inatumia fedha nyingi kupanda miti”.
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
Novemba 18,2024.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa