WANAUME (CMF) wa Kanisa la Tanzania Assemblies Of God (TAG) wanaadhimisha wiki lao kwa kufanya huduma mbalimbali za kiroho na Kimwili kote Nchini.
Wanaume kutoka Kanisa la TAG Madaba wametembelea kituo cha Afya Madaba wametoa zawadi mbalimbali kwa wanawake waliojifungua na wanaotarajia kujifungua katika kituo hicho na kuchangia damu.
Mtaalam wa Maabara katika kituo hicho Elvida Eliushu amewashukuru kwa zoezi walililolifanya la kutoa zawadi kwa wanawake waliojifungua na wanaotarajia kujifungua pamoja na kuchangia damu ambayo itawasaidia wagonjwa wengine.
“Sisi kama wahudumu wa Afya tumefurahia na mmetutia moyo sana Damu hiyo itawasaida wagonjwa,wajawazito,na hata wale ambao hawana ndugu”
Hata hivyo mtaalam huyo amesema kuna Madaktari bingwa watafanya huduma mabalimbali katika Hospitali ya Wilaya hivyo damu itahitajika sana zoezi hilo litaanza Mei 6 hadi 10 kuanzia saa mbili kamili asubuhi na kuendelea.
Naye Mchungaji Msaidizi Paulo motela katika zoezi walilofanya katika kituo hicho amewashukuru Madaktari kwa kuwapa nafasi ya kuchangia damu na kutoa zawadi kwa wanawake pamoja na kuwafanyia maombi.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Madaba
Mei 4,2024.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa