WALIMU Halmashauri ya Madaba wameaswa kuepuka mikopo kausha damu badala yake waheshimu mshahara ambao wanaupata mwisho wa mwezi.
Hayo amesema Mhe.Diwani wa Kata ya Matumbi Valentino Mtemauti akimwakilisha Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Madaba Teofanes Mlelwa katika kikao cha tathimini ya matokeo ya mitihani ya Kitaifa kwa shule za msingi mwaka 2023 iliyoambatana na sherehe ya kuwapongeza walimu hao kwa kuwapa zawadi mbalimbali na wanafunzi waliofanya vizuri.
“kopa mkopo kwa malengo siyo unakopa bila malengo mwisho wake unawekwa mahabusu mshahara wako unaopata si haba uheshimu”.
Aidha Mtemauti amewapongeza walimu kwa jitihada walizofanya na kuhakikisha Halmashauri ya Madaba inakuwa yakwanza kimkoa kwa matokeo ya darasa la saba na darasa la nne mwaka 2023.
Mtemauti amempongeza Mbunge wa Jimbo la Madaba,Mwenyekiti wa Halmashauri ,Mkurugenzi mtendaji kwa kuwa chachu ya kusababisha matokeo mazuri katika Halmashauri ya Madaba.
Kutoka kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Madaba
Mei 17,2024.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa