Afisa Elimu awali na msingi Saada chwaya Halmashauri ya Wilaya ya Madaba amefungua mafunzo ya Walimu wa awali yanayoendelea kwa mda wa siku nne kupitia mradi wa BOOST.
Akizungumza na walimu hao Chwaya amesema kupitia mafunzo hayo ya ufundishaji wa elimu ya awali Serikali inaboresha elimu ikiwa nyumba nzuri kuanza kujengwa katika msingi.
“Msingi ukiwa imara na nyumba inakuwa imara mwanafunzi akianza kutambua kwa kuandika akiwa darasa la awali,darasa la kwanza hatakuwa na shida atakuwa anaongezewa maarifa Serikali imetudhamini kutoka ngazi ya Taifa hadi Wilaya baada ya mafunzo haya tukafanye kazi”.
Amesema dhamana kubwa ambayo Serikali imetoa ni kuhakikisha mafunzo haya yanatoa matokeo chanya hata wakaguzi watakapopita kufanya ukaguzi wakute walimu wameiva na wanafanya kazi kama ilivyokusudiwa.
“Niwaombe tuwe makini kuchangia,kushiriki kile ambacho tunaelekezwa na wakufunzi wetu ili tupate kile ambacho Serikali imekusudia na kukifanyia kazi”.
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
Januari 18,2024.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa