SERIKALI ya awamu ya sita imeleta fedha zaidi ya shilingi Bilioni 3 kwaajili ya ujenzi wa Hospitali ya Wilaya Halmashauri ya Madaba.
Kwa kipindi cha mwaka wa fedha 2022/2023 Halmashauri ilipokea kiasi cha shilingi milioni 834 kwaajili ya ujenzi wa Hospitali hiyo na kufikia hatua ya ukamilishaji.
Hata hivyo kwa mwaka wa fedha 2023/2024 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba imepokea kiasi cha shilingi Milioni 900 kwaajili ya utekelezaji wa ujenzi wa Hospitali ya Wilaya,ukamilishaji wa Zahanati ya Mahanje,pamoja na Zahanati ya Ifinga.
Aidha utekelezaji wa wa Zahanati ya Mahanje umekamilika na mradi unatoa huduma kwa wananchi,ukamilishaji wa Zahanati ya Ifinga unaendelea pamoja na Hospitali ya Wilaya.
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Madaba
Januari 22,2024.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa