Benki ya NMB imetoa vifaa vyenye thahamani ya zaidi ya shilingi Milioni 49 katika seka ya afya na Elimu Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.
Akitoa taarifa hiyo Meneja wa Benki ya NMB kanda ya kusini Lipa Abel kuwa vifaa hivyo vimetolewa ni vitanda 50,magodora 50 katika hospitali ya Wilaya ya Madaba na madawati 50 na viti 50 katika shule ya Sekondari Matetereka.
“Tunashukuru kwa kuwa NMB ni mahali sahihi pakukimbilia inaonyesha jinsi uthamini wa mchango wetu kwenu kama benki katika kuchangia maendeleo katika Halmashauri ya Wilaya hii ya Madaba”.
Hata hivyo amesema vifaa vilivyokabidhiwa leo nimoja ya ushiriki katika maendeleo ya jamii na NMB ni benki inayoongoza Tanzania ikiwa wanao wajibu wa kuhakikisha jamii inafaidika katika faida inayopata katika benki ya NMB.
Amesema kwa miaka mingi Benki ya NMB imekuwa ikichangia maendeleo katika miradi ya elimu kwa utoaji wa madawati na vifaa vya kuezekea na katika sekta ya afya inachangia vitanda na magodoro na vifaa vya matibabu pamoja na kusaidia majanga yanayotokea Nchini.
“Mgeni rasmi benki ya NMB imekuwa mstari wa mbele katika kuchangia jamii kwa lengo la kurejesha faida yetu ikiwa ni zaidi ya miaka saba mfululizo tumetenga asilimia moja kwa kuchangia maendeleo ya jamii.
“Benki ya NMB inaongoza nchini ikiwa na matawi zaidi ya 231,mashine za ATM 780 Nchi nzima mawakala zaidi ya 20,000 na tumeanzisha huduma vijijini na kusaidia wananchi wanaweza kupata huduma za benki bila kufika mjini.
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano halmashauri ya Madaba
Novemba 18,2024.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa