HALMASHAURI ya Wilaya ya Madaba wamefanya mkutano maalum wa baraza la Madiwani na kuridhia kutoa eneo la Maliasili Mahenge kwa Wakala wa Misitu Tanzania (TFS).
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Sajidu Idrisa Mohamed akisoma taarifa amesema wajumbe kamati ya fedha waliagiza kamaya wataalam (CMT) ikae na kupendekeza mradi mmoja wenye tija ya kuongeza mapato ya Halmashauri na kuwasilisha kwa Wakala wa Misitu.
Aidha amesema kamati ya wataalam walipendekeza na kuandaa andiko la mradi wa Soko la Mbao lenye thamani ya shilingi Milioni 253,500,000 kwa awamu mbili.
Amesema fedha hizo zitatolewa awamu ya kwanza milioni 87 ujenzi wa miundombinu na awamu ya pili Milioni 16,500,000 ujenzi wa uzio na 150 ununuzi na kufunga mzani.
“ Utekelezaji wa mradi huo wa soko la mbao utarahisisha ukusanyaji wa maduhuli,upatikanaji wa taarifa ya soko,ubora wa mbao kwa wanunuzi,urahisi wa upatikanaji wa takwimu za biashara ya mazao ya misitu,ajira mbalimbali kwa vijana”.
Kwa upande wake Meneja wa TFS Songea Issa Haruna Mlela amelishukuru baraza hilo kwa kuridhia ombi la kupatiwa eneo la maliasili Mahenge.
“Tunawashukuru sana kwa kuridhia ombi letu tunawaahidi tutakuwa na mahusiano mazuri na tutaendelea kuboresha na tutafanya kazi kama timu”.
Kutoka Kitengo cha Mawsailiano Halmashauri ya Madaba
Juni 7,2024.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa