AFISA Mazingira Halmashauri ya Wilaya ya Madaba Grolia Mrisho ametoa elimu ya matumizi ya Nishati mbadala katika maadhimisho ya siku ya wajane.
Akitoa elimu hiyo amesema katika Halmashauri ya Wilaya ya Madaba nishati inayotumika kwa asilimia kubwa ni kuni na mkaa hali ambayo inasababisha uharibifu wa mazingira.
“Hali ya tabia ya nchi imebadiliaka sana vipindi vya mvua vinakuwa vifupi,halafu mvua zinanyesha kubwa kwa wakati mmoja na kiangazi kwa mdara mrefu na kuathiri mazingira”.
Mrisho amesema moja ya sababu ya kuathirika kwa mazingira ni matumizi ya nishati ya mkaa na ukataji wa miti hovyo unapelekea kuchangia ongezeko la uharibifu wa mazingira na kusababisha mafuriko na mmomonyoko wa ardhi.
“Serikali ikaona kunahaja ya wananchi wake kutumia njia mbadala ya nishati ambayo itapunguza athari za mazingira”.
Amesema nishati ambadala ambayo haikaushi dunia na haichafui mazingira ni jua, mimea iliyokufa,kinyesi cha wanyama,upepo,umeme na gesi.
“kupitia elimu hii naomba tukawaambie na akina mama wengine wazijue nishati mbadala ambazo haziharibu mazingira yetu”.
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
Juni 27,2024.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa