KAIMU Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Anitha Makota amegawa vifaa kwa Watoto wanaoishi katika mazingira magumu katika Kata tano za Halmashauri ya Madaba vyenye thamani ya shilingi laki tano.
Akizungumza ofisini kwake mara baada ya kukagua kikundi cha watu wenye Ulemavu kata ya Mateteleka chenye watu kumi na mbili wa jinsia totauti na kutembelea wajane Kata ya Mkongotema.
Makota amesema Lengo la kuonana na Wajane hao ni kuweza kuwatambua na kuwatia moyo baada ya kupoteza wenza wao na kuwaelekeza fursa zilizopo Halmashauri ya Madaba ikiwemo mikopo ya asilimi 10 kwa wanawake.
Hata hivyo amezungumzia jinsi walivyo tekeleza siku ya Mtoto wa Afrika iliyofanyika tarehe 16 Juni 2021 katika Kata ya Lituta ilihudhuriwa na Mwenyekiti wa Halmashauri na viongozi wataka na Kijiji.
“Ndani ya hii Kata ya Lituta tuliendelea kufuatilia Walevavu na kuwagundua na tumeendelea kuwalea ni sehemu ya jukumu letu kuhakikisha kwamba ile miradi wanayoindeleza inakuwa endelevu na kila Kata tumehakikisha usalama wa watoto unaenda sawasawa kama unavyotakiwa”.
Makota akizungumzia mikakati waliyoweka katika idara hiyo amesema kuhakikisha wanaleta Umoja na Mshikamano ili kuendelea kufanya kazi kwa usahihi.
“Tunamuenzi Mh. Hayati Rais Magufuli alihimiza umoja mshikamano upendo na kufanya kazi kwa bidii na kwa hali zote hata Rais wetu Samia anasisitiza kufanya kazi kwa bidii kwa kujitoa na kuhakikisha Taifa letu linakuwa na Maendeleo”.
Amesema mkakati wa asilimia 10 kama lilivyoelekezwa atahakikisha linaelekezwa kwa walengwa Wanawake,walemavu,na vijana kwa kuwaibulia miradi mikubwa na yenye tija itakayowawezesha kiuchumi.
Mkakati wa kupinga ukatili wa kijinsia amesema wameendelea kutoa elimu katika shule mbalimbali na mitaa na mara baada ya shule kufunguliwa watatoa kampeni inayopinga Ukatili na kuelekeza namna ya kutoa taarifa.
Mkuu wa Idara pamoja na timu yake amesema wamejipanga kutokomeza mimba za Utotoni ikiwepo Halmashauri ya Madaba watoto wanapata Mimba wakiwa na umri mdogo kwa asilimia kubwa nao wamejipanga kutoa elimu kwa wazazi na kuhakikisha watoto hao wanatuzwa.
Amesema pia katika swala zima la kupunguza maambukizi ya Virusi vya UKIMWI wamejipanga kuwahimiza walioathirika kuendelea kutumia dawa na kwenda kliniki, ikiwemo akinamama wajawazito kwenda hospitali na kucheki afya zao mapema.
Amesisitiza kwa wanawake kuungana na kuibua miradi yenye tija ili iweze kuwaletea maendeleo katika Halmashauri ya Madaba ilikuhakikisha wanajifunza,wanajituma na kujitegemea.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Afisa Habari Halmashauri ya Mdaba
Juni 28,2021
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa