AFISA wa Ofisi ya Maadili Kanda ya Kusini Samweli Omary ametoa Semina ya Maadili katika Baraza la Madiwani Halmashauri ya Madaba lililofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya Mkurugenzi.
Akizungumza katika Baraza hilo ameeleza faida ya Kiongozi na Mtumishi wa Umma kuwa mwadilifu katika utumishi ni pamoja na kulinda heshima na haiba kwa kiongozi au mtumishi.
Amesema uadilifu huleta umoja na mshikamano kwa kuleta mahusiano mazuri,utendaji bora pamoja na utoaji wa huduma bora na kupunguza malalamiko yasiyo ya lazima kutoka kwa wale unaowahudumia.
“Uadilifu kama viongozi na watumishi wa Umma unawawezesha kuwa na matumizi sahihi na mazuri ya rasilimali za Umma huwezi kuwa na kashifa za ufisadi,ubadhilifu wa fedha za Umma”.
Hata hivyo amesema uandilifu husaidia kulinda hadhi ya Taasisi na Serikali,inasaidia kuepuka migogoro mahali pa kazi na sehemu nyingine pamoja na kutenda haki na kudumisha usawa.
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Madaba
Januari 31,2024.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa