AFISA Elimu Mkoa wa Ruvuma Maria Makala ametoa rai kwa Walimu wakuu na Maafisa Elimu Kata kufanyia kazi mapungufu katika swala nzima la ufundishaji.
Hayo amesema katika kikao kazi cha wadau wa Elimu Jifunze uelewe kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Madaba amesema mwalimu yeyote kama anamapungufu aelekezwe.
“Kimsingi tunanafasi kubwa ya kwenda kuwaelekeza wale walimu ambao tunaona hawapo vizuri katika ufundishaji tumeona mapengo yalipo kila mnapofanya upimaji bahati nzuri matokeo mmeyaona”.
Makala amewaomba walimu wakuu na Maafisa Elimu Kata kwenda kukaa na walimu wao kutatua changamoto zilizopo katika Shule zao kufuatia Mkoa wa Ruvuma kupitia matokeo ya mwaka 2022 kuwa wamwisho Kitaifa.
Hata hivyo amesema miongozo imetolewa na mafunzo mengi kwa walimu hivyo ameomba ufaulu upande siyo kushuka kwasababu Serikali imetambua umuhimu wa kuwa na malengo ya kuboresha ili walimu wafanye kazi katika mazingira yanayoridhisha.
“ Tunaomba walimu kuu muwe karibu na walimu wenu wakati mwingine hata kwa kuongea nao pengine wanamatatizo ya kisaikolojia hata maswala ya kawaida kama anachangamoto msaidie ili wawe na moyo wa kufanya kazi kwa bidii”.
Makala amewaasa walimu kutumia Vishikwambi kwa matumizi sahihi ya kujifunzia na kufundishia kama Serikali ilivyoelekeza na vifaa vilivyotolewa kwaajili ya wanafunzi wenye mahitaji maalumu.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Madaba
Januari 26,2023.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa