MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge ametoa maagizo ya mfumo wa ugavi wa Bidhaa za afya.
Hayo amesema katika kikao kazi cha viongozi wa Serikali wa Mkoa wa Ruvuma kilichofanyika jana katika ukumbi wa Manispaa ya Songea.
Ibuge amesema lengo la kikao hicho ni kukumbushana kuhusu mfumo wa utoaji wa huduma bora za afya kwa wananchi na hatimaye kuimarisha uwajibikaji wa pamoja katika uendeshaji,utoaji,ufuatiliaji na usimamizi wa huduma za afya zikiwemo dawa na vitendanishi katika Mkoa wa Ruvuma.
“Usimamizi wa huduma za afya katika maeneo yetu unaofanywa na viongozi kwa kushirikiana na wananchi unaofanywa kupitia nyenzo za vikao kwa mujibu wa miongozo iliyotolewa na Wizara ya afya,Maendeleo ya jamii,Jinsia wazee na watoto”.
“ katika kikao hiki mmepata fursa ya kuzielewa nyenzo taratibu na mifumo iliyopo ili kazi ya usimamizi,ufuatiliaji na tathimini iweze kufanywa kwa umahiri mkubwa zaidi,baadhi ya mifumo hiyo ni kamati za Hospitali,Bodi za huduma za afya za Halmashauri na kamati za afya ya msingi(PHC)”
Ibuge akitoa Maelekezo kwa Viongozi hawa amesema wahakikishe vikao vinafanyika kwa mujibu wa kalenda ya vikao vya kamati na maazimio yafanyiwe kazi na Mganga mkuu wa Mkoa kupitia katibu tawala wa Mkoa atawasilisha taarifa za utekelezaji kwa mkuu wa Mkoa kila robo mwaka.
Ifikapo Septemba Mosi 2021 vituo vyote vya kutolea huduma za afya vya umma viwe vimefungwa mfumo ya kukusanya mapato (GOTHOMIS) bila kukosa na tarehe 2 septemba niwe nimepata taarifa ya utekelezaji.
Amesema mapato na matumizi ya vyanzo katika Halmashauri yawe yanajadiliwa katika vikao vyote vya kisheria kuanzia ngazi ya kituo hadi balaza la Madiwani hususani kamati za vituo vya kutolea Huduma za Afya Bodi za huduma za Afya za Halmashauri.
Hata hivyo amesema Moja ya kigezo muhimu kitakachotumika kuangalia ufanisi wa ukusanyaji wa mapato ya Halmashauri katika Mkoa wa Ruvuma kuanzia mwaka wa fedha 2021/2022 lazikma kufikia zaidi ya asilimia 80 ya mapato ya vyanzo vya sekta ya afya (NCHF,NCHF,na user fees)
Halmashauri zihakikishe vituo vyote vya kutolea Huduma za afya Umma kama Zahanati,Vituo vya afya na Hospitali vinatumika kila mwezi kwa wakati madai (claims) na mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya(NHIF)
Amesema Halmashauri zihakikishe uhamasishaji mkubwa wa jamii kujiunga na mfuko wa afya ya Jamii na uboreshaji wa (iCHF)hadi sasa Mkoa umefikia kuandikisha kaya zilizo hai 11,820 sawa na asilimia 3.3 lengo ni kufikia 180,085 sawa na asilimia 50 na halmashauri ziwe na bajeti na mipango ya kweli inayoakisi mapato halisi ya sekta ya afya na hatimaye kupanua wigo wa huduma bora ya afya.
Dr.Kanga amesema mfuko wa iCHF mkoani Ruvuma ulianza kutekelezwa mwaka 2019,ambapo kitaifa Mkoa ulishika nafasi ya mwisho ambapo hivi sasa Mkoa umepanda hadi kufikia nafasi ya 11 kitaifa na kwamba kikao kazi hicho kitaongeza ufanisi na tija.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Afisa Habari Halmashauri ya Madaba
Mai 11,2021
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa