• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
MADABA DISTRICT COUNCIL
MADABA DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Madaba

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Department and Section
  • Investment
  • Huduma
    • Huduma ya Kwanza
    • Huduma ya Pili
  • Councillors
  • Miradi
    • Mradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa
    • Matukio
  • Divisheni

MAKAA ya Mawe Ruvuma yaingiza bilioni 400 na kutoa ajira 700

Posted on: November 2nd, 2020

MADINI ya makaa ya mawe yanayochimbwa mkoani Ruvuma yameingiza zaidi ya shilingi bilioni 400 na kutengeneza ajira za watanzania zaidi ya 700.

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme amesema kiasi hicho  cha fedha kimepatikana kutokana na mauzo ya madini ya makaa ya mawe zaidi ya tani milioni  3.3 ambayo yameuzwa kuanzia Agosti 2017 hadi Oktoba 2020.

Amesema uchimbaji wa madini ya makaa ya mawe unafanyika katika wilaya za Songea ,Mbinga na Nyasa na kwamba Mkoa wa Ruvuma una hazina kubwa ya mashapo ya madini ya makaa ya mawe yaliyofanyiwa utafiti na kampuni tatu kubwa za uchimbaji.

“Kwa mujibu wa utafiti huo,Mkoa wa Ruvuma una mashapo ya makaa ya mawe zaidi ya tani  milioni 457,mashapo hayo tulionayo,tunaweza kufanya uchimbaji kwa miaka 718 bila kumaliza hazina hii’’,amesema Mndeme.

Hata hivyo Mndeme amesema katika kipindi cha mwaka 2019/2020  zaidi ya tani 636,000 za makaa ya mawe ziliuzwa ndani na nje ya nchi.

Amesema Mkoa wa Ruvuma umebarikiwa kuwa na madini ya aina mbalimbali yakiwemo madini ya vito na dhahabu ambayo yanachimbwa kwa wingi katika wilaya za Tunduru,Songea ,Mbinga na Nyasa.

Mndeme amesema madini ya vito na dhahabu kuanzia Mei 2019  Mkoa ulianzisha masoko ya madini katika wilaya za Tunduru na Songea ambapo hadi sasa zimeuzwa gramu zaidi ya milioni moja zenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni saba 7.7 na kwamba watanzania  zaidi ya 1000 wamepata ajira kwenye za uchimbaji  wa madini hayo.

Amesema Mkoa wa Ruvuma umejenga kituo cha umahiri wa madini ambacho kitawawezesha wachimbaji kupata elimu ya uchimbaji na utambuzi wa madini hayo.

Imeandikwa na Albano Midelo

Afisa Habari Mkoa wa Ruvuma

Novemba 2,2020        

Matangazo

  • VIGEZO vya kupata Lesen May 17, 2022
  • Angalia zote

Matangazo Mapya

  • HALMASHAURI YA WILAYA YA MADABA YAPONGEZWA KWA KUPATA HATI SAFI KWA MWAKA WA FEDHA 2023/2024.

    June 19, 2025
  • UJENZI WA MADARASA 2 NA MATUNDU 6 YA VYOO SHULE YA MSINGI KIPINGO WAKAMILIKA KWA ASILIMIA 100

    May 30, 2025
  • Uboreshaji wa Daftari la kudumu jimbo la Madaba

    January 20, 2025
  • Jitokeze kujiandikisha

    January 20, 2025
  • Angalia zote

Video

WADAU WATOA MAONI JUU YA MAADILI KWA VIJANA
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Ruvuma-webportal
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Nyasa District Council
  • Ega Website
  • Namtumbo District Council
  • Mbinga Town Cuncil
  • Songea District Council
  • Songea Municipal Council

Kurasa Mashuhuru

  • NECTA
  • Tanzania Revenue Authority
  • Tanzania Forest Agency
  • Watumishi portal
  • Livestock Training Agency (LITA) Madaba
  • Parliament

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana Nasi

    MADABA - RUVUMA

    Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA

    Simu: 0252951052

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: ded@madabadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Falagha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya Mahali
    • Huduma

Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa