MRADI wa ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa katika Shule ya Sekondari Madaba uliotekelezwa kwa shilingi milioni 40 umekamilika kwa asilimia 100.
Akisoma taarifa hiyo Mkuu wa Shule ya Sekondari Madaba Kevin Kalesa kwa wataalamu kutoka ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma walipotembelea Madarasa hayo amesema ujenzi ulianza Octoba 18,2022.
“Mradi umekamilika kuanzia Desemba 18,2022 kwa asilimia 100 kwa viti 50 na meza 50 kwa fedha yote iliyotengwa kutoka Serikali kuu”.
Kalesa amezitaja faida za vyumba vya madarasa hayo ikiwa pamoja na kupunguza tatizo la madarasa,kuwezesha wanafunzi waliojiunga na kidato cha kwanza 2023,uwepo wa samani bora kwa wanafunzi wakati wa kujifunza,kuamsha ari ya wanafunzi kujifunza.
Mkuu wa Shule ametoa shukrani za dhati kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa ajili ya kuleta fedha za mradi wa Madarasa ambayo yanaendelea kuleta tija ya kuboresha mazingira ya kujifunzia.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa