MBUNGE Jimbo la Madaba Mhe.Joseph Mhagama ametembelea na kukagua mradi wa Maji katika Kijiji cha Ngadinda Kata ya Gumbiro Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.
Mhandisi wa Ruwasa Wilaya ya Songea Sheila Kimweli akisoma taarifa katika ziara ya Mbunge iliyojumuisha viongozi wa chama cha Mapinduzi amesema mradi huo unatekelezwa kwa zaidi ya shilingi bilioni Moja kwa kutumia force account.
“Mradi huu unatekelezwa kupitia mradi wa lipa kwa matokeo EP4R na ulianza rasmi februari 25,2024”.
Mbunge wa Jimbo hilo amewashukuru wananchi kwa ufuatiliaji wa mradi huo na Ruwasa kwa kutoa ushirikiano wanaotoa katika Jimbo la Madaba.
“Ngumbiro tunabahati tumepata Diwani mzalendo anayeweza kupambana mpaka tunafika mahali anaweza kupata miradi mingi “.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
Julai 24,2024.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa