HALMASHAURI ya Wilaya ya Madaba Kitaifa imeshika nafasi ya 4 katika zoezi la afua za Lishe kwa kutenga fedha kwa kila mtoto kwa shilingi elfu nne kwa miaka miwili mfululizo.
Hayo amesema Mkuu wa Wilaya ya Songea Wilman Ndile katika Kikao cha Liche cha robo ya kwanza 2023/2024 kilichofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Mkurugenzi na kuhudhuliwa na wajumbe mbalimbali.
“Kitaifa Halmashauri ya Wilaya ya Madaba imefanya vizuri kwa usimamizi wa Fedha na kufikia kutoa kwa kila mtoto shilingi elfu 4,000/= hii ni hatua muhimu sana kama alivyoagiza Mh. Rais Samia”
Ndile amempongeza Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Sajidu Idrisa Mohamed kwa kuzingatia na kuvuka malengo ya Serikali ambapo imeagiza kila mtoto atengewe kiasi cha shilingi 1,000/= na kufikia shilingi 4,000/=.
Ndile amewaagiza watendaji Kata kuhamasisha wananchi kufanya mazoezi ya viungo ili kuimarisha Afya zao na kuepukana na Magonjwa na uzito uliokithiri.
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
Oktoba 25,2023.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa