Kamati ya Fedha Halmashauri ya Wilaya ya Madaba wametembelea na kukagua miradi mbalimbali ukiwemo mradi wa soko linalojengwa kwa mradi wa TASAF kwa shilingi Milioni 190.
Akisoma taarifa hiyo Mtendaji wa Kijiji cha Lituta Leokadia Msigwa amesema hadi kufikia sasa kiasi cha fedha zilizotumika ni zaidi ya shilingi Milioni 113 kwaajili ya ununuzi wa vifaa vya viwandani na visivyo vya viwandani pamoja na kulipa mafundi.
Hata hivyo amesema mradi huo unatarajia kukamilika Februari 20,2024 ikiwa mradi utaleta faida kwa wananchi wa Madaba kwa kupanua wigo wa upatikanaji wa bidhaa.
Kupunguza gharama za wananchi kwenda kutafuta mahitaji yao katika Wilaya za jirani na kujipatia mahitaji yao kiurahisi.
“Soko litasaidia kuongeza mapato ya Halmshauri na kijiji,pamoja na kuboresha mazingira rafiki kwa wafanyabiashara na wananchi”,
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Madaba
Januari 23,2024.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa