WADAU wa Elimu Jifunze uelewe (RTI) wamefanya kikao kazi na Idara ya Elimu Msingi,Maafisa Elimu Kata ,Wadhibiti ubora pamoja na Walimu Wakuu Halmashauri ya Madaba.
Mratibu wa Elimu Jifunze uelewe Paul Kijaji akizungumza mara baada ya kumaliza kikao kilichofanyika katika ukumbi wa Jengo la Halmashauri ya Madaba amesema wadau wa elimu wamekutana na watalaamu wa Elimu kwaajili ya kufanya tathimini ya matokeo ya,darasa la nne na darasa la saba mwaka 2022.
Kijaji amesema kufuatia matokeo ya 2022 kuwa mabaya na kupelekea Mkoa wa Ruvuma kuwa wa mwisho ikiwa wao ni wadau wa Elimu wameweka mikakati kwa maafisa Elimu Kata na Walimu wa kuu kukaa kwa pamoja na kuanza kwa upya mwaka 2023 ili matokeo yaweze kuwa mazuri.
“Tumefanya kikao cha tathimini na tumeweka mikakati ili kwa kila mwalimu Mkuu hata wale wa chini watajua namna ya kufanya itasaidia kubaini wanafunzi ambao hawana uelewa na watapatiwa msaada kwa wakati na kwa haraka”.
Afia Elimu msingi Elimu Maalumu Halmashauri ya Madaba Teddy Sanga katika kikao hicho amesisitiza utekelezaji wa hadidu za lejea zilizopo kwenye mkataba ambao kila mwalimu ameusaini.
“Ni Mikoa michache sana ambayo tumepata bahati na fursa ya kuwa na huo mradi wa jifune uelewe kuna Mkoa wa Iringa,Ruvuma,Morogoro na Mtwara kati ya Mikoa 26”.
Hata hivyo amesema Mkoa wa Ruvuma ni kinara kwa unafanya uzalishaji wa chakula miaka minne mfululizo na kiashilia kinachofanya mtoto aweze kufanya vizuri darasani ni afya bora inayotokana na Lishe bora kinacho hitajika ni kusimamia kwa weledi na utekelezaji kwasababu chakula Ruvuma kipo cha kutosha.
“Jifunze uelewe waliwapatia walimu wakuu na Maafisa Elimu Kata Vishikwambi kabla ya zoezi la Sensa kwaajili ya utendaji kazi,kwasababu tumeamua,tumepewa maelekezo,tumefanya tathimini naomba tukalete mabadiliko chanya ya kupata matokea mazuri huku wadau wetu Jifunze uelewe wakitushika mkono”.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Madaba
Januari 26,2023.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa