HALMASHAURI ya Wilaya ya Madaba imetoa mkopo wa Guta kwa kikundi cha Mothers group lenye thamani ya shilingi milioni sita na laki saba (6,700,000/=) iliyotokana na mapato ya ndani.
Akikabidhi guta hilo kwa kikundi hicho Mwenyekiti wa Hamashauri ya Madaba Teofanes Mlelwa amewaasa wanakikundi hao suala la uaminifu wa marejesho ya mkopo waliopewa ili waweze kukopeshwa tena.
“Kikubwa tambueni fedha za Halmashauri tunazo wakopesha siyo zawadi kwasababu wengine wakikopeshwa hawarudishi wakidaiwa wanasema ni mali yao mpaka tumeanza kupelekana kwenye vyombo vya sheria”.
Hata hivyo amesema kupitia mkopo huo wahakikishe wanafikia malengo waliyokusudia maana Halmashauri ya Madaba inawajali sana wanawake,vijana na wenyeulemavu ili na wengine waweze kukopa.
Kaimu Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Bashiru Mgwasa amesema kuwa guta ni mali ya Halmashauri ya Madaba mpaka pale watakapo maliza Mkopo wao wa shilingi milioni sita na laki saba zilizotumika kununulia.
“Sasahivi umiliki utakuwa wa pande Mbili Mothers group na upande wa Halmashauri ya Madaba mtakapomaliza tutahamisha umiliki utabaki wa kikundi chenu”.
Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Olaph Pili amemponge Mwenyekiti wa Halmashauri na Mkurugenzi pamoja na wataalamu kwa kusimamia mapato ya ndani na kuhakikisha vikundi vinakopeshwa.
Mhasibu wa kikundi hicho kwa niaba ya wenzake Stela Mkinga amewashukuru viongo wa Halamshauri kwa kuwapatia Mkopo na ameahidi kurejesha Mkopo huo kwa uaminifu na kwa wakati.
Kikundi cha mothers group mwaka 2021 walipewa mkopo wa shilingi milioni 10 kutokana na mapato ya ndani ya Halmashauri.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Halmashauri ya Madaba
Januari 27,2023.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa