MKUU wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya Madaba Anitha Makota pamoja na Afisa Ustawi wa Jamii Shani Kambuga wametoa Elimu ya ukatili wa Kijinsia kwa Wanawake,Wanaume pamoja na watoto Jijiji cha Magingo Kata ya Mkongotema Halmashauri ya Madaba
Kufuatia kampeni ya siku 16 ya kupinga ukatili wa Kijinsia Tanzania Nzima amewaasa wananchi hao kutofumbia macho mambo yakikatili ambayo husababisha madhara ya kifamilia na kudhorotesha Taifa.
Makota ametoa rai kwa wananchi hao kuhakikisha wanapokutana na Changamoto yoyote ya unyanyasaji huo wasifumbie macho bali watoe taarifa katika sehemu husika ikiwemo ofisi ya kijiji,ofisi ya Ustawi wa jamii pamoja na ofisi ya serikali za Mitaa.
‘’Kwasababu mda mwingine kuna mambo yanatokea lakini hatupati taarifa hakikisheni mnatoa taarifa ili kuhakikisha tunachukua hatua”.
Afisa ustawi wa Jamii Shani Kambuga ameelezea maana ya ukatili wa kijinsi ni kitendo anachofanyiwa mwanaume,mwanamke au mtoto na kupelekea kuathilika kisaikolojia.
Kambuga amesema ukatili wa kimwili ni kitendo cha mama kupigwa au mwanaume kukatwa kwa ncha kali, au kutukanwa kwa kuitwa majina ya wanyama.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Madaba
Desemba 3,2022.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa