3. MAENEO YA UWEKEZAJI YALIYOTAMBULIKA YALIYOPO KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA MADABA
ENEO LA EKARI 400 KWENYE MJI WA MADABA
Eneo hili la ekari 400 lipo katika kitongoji cha Ifugwa kijiji cha Madaba kilomita 10 kutoka barabara kuu ya Songea-Njombe kwenye mji wa Madaba ukielekea wilaya ya Ludewa. Ni eneo lililotengwa kwa ajili ya uwekezaji wa viwanda vya aina mbalimbali. Mwekezaji yeyote anakaribishwa na atapewa eneo la kujenga kiwanda/shughuli yoyote atakayohitaji. Aidha Halmashauri inaendelea kupima viwanja katika vijiji vyote vinavyozunguka Mji wa Madaba ambapo tunarajia kutenga maeneo mengine ya uwekezaji.
ENEO LA ITOMBOLOLO KIJIJI CHA MKONGOTEMA
Eneo hili la hekta 2000 lipo katika kijiji cha Mkongotema mpakani na kijiji cha Lutukila kandokando ya barabara kuu ya Songea - Njombe. Ni eneo lililotengwa kwa ajili ya shughuli za uwekezaji hasa viwanda vya kuchakata/kuongeza thamani ya mazao kama vile mahindi, tangawizi na mazao mengine. Eneo hili ni mali ya kijiji hivyo yeyote anayehitaji, Halmashauri na Kijiji watahakikisha Mwekezaji anapata eneo analohitaji kwa ajili ya uwekezaji ili wananchi wanufaike na fursa za kazi zitakazojitokeza.
SHAMBA LA MIFUGO HEKTA 4,200 (EKARI 10,500)
Eneo hili ni mali ya Wizara ya Mifugo lipo kandokando ya Barabara kuu ya Songea – Njombe. Halmashauri ya Madaba inalitunza na kulitumia. Wawekezaji wanakaribishwa kwa ajili ya shughuli za ufugaji wa mifugo (Ng’ombe). Kwa sasa kuna wafugaji waliokodishwa vitalu 16. Hivyo bado kuna nafasi ya kupokea wafugaji wengine wanaohitaji kufuga kwenye vitalu 8. Aidha eneo limepitiwa na mto mkubwa unaowezesha kutumika kwa uzalishaji wa chakula (Nyasi) cha mifugo.
ENEO LA HALMASHAURI EKARI 500
Halmashauri inamiliki eneo lake la ekari 500 lililopo KM 18 kutoka barabara kuu ya Songea – Njombe ukielekea kijiji cha Ifinga. Eneo hili lipo tayari kwa Mwekezaji yeyote kuwekeza kwa shughuli za kilimo, hasa kilimo cha Miti, Kahawa na mazao mengine yanayoendana nayo.
MAPOROMOKO YA KUZALISHA UMEME WA MAJI
Halmashauri YA wilaya ya Madaba ina maporomoko yanayoweza kuzalisha umeme. Maporomoko haya ni pamoja na Masigira, Lipupuma na Lingatunda. Waekezaji wanakaribishwa kuwekeza.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa