Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Madaba Sajidu Idrisa Mohamed amekagua mradi wa ujenzi wa Madarasa ya Boost yakiwemo madarasa 2 ya awali ya mfano katika shule ya Msingi Ifugwa.
Madarasa hayo Ya mfano yatajengwa kwa shilingi Milioni 66,300,000/= pamoja na matundu ya vyoo 6 ikiwa shule ya Msingi Mahanje yatajengwa Madarasa 2 na matundu ya vyoo 3 kwa shilingi Milioni 53,100,000/=.
Hata hivyo katika mradi wa Boost katika Halmashauri ya Madaba shule za Msingi 6 zimepata fedha kwaajili ya ujenzi wa Madarasa ikiwa Shule ya Msingi Lipupuma itajengwa Madarasa 8 na na jengo la Utawala shilingi Milioni 331,600,000/= zitatumika katika ujenzi huo,Shule ya Msingi Turihani Milioni 53,100,000/= zitajenga madara 2 na matundu ya vyoo 3 pamoja na Shule ya Msingi Ngembambili Shilingi Milioni 53,100,000/= zitajenga madarasa 2 na matundu ya vyoo 3.
Mkurugenzi ameagiza kuhakikisha ujenzi huo unakamilika kwa wakati na kwa ubora kabla ya kumaliza mwaka wa fedha 2022/2023.
Kutoka kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Madaba
Mei 24,2023.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa