SERIKALI imeleta fedha kiasi cha shilingi Milioni 141 kwaajili ya ujenzi wa Bweni katika Shule ya Sekondari Ifinga.
Hayo amesema Mkuu wa Wilaya ya Songea Wilman Ndile alipokuwa akizungumza na wananchi wa Kata yaLituta na Mahanje wakati wa uzinduzi wa Soko la Kisasa linalojengwa kupitia mradi wa TASAF.
“ Serikali inafikilia kujenga miundo mbinu Mbunge wenu amepambana ndiomana miundombinu inaboreshwa,na tumeletewa fedha Milioni 141 kwaajili ya ujezi wa Bweni Ifinga”.
Ndile amesema ujenzi wa Bweni katika Shule ya Sekondari Ifinga litasaidia wanafunzi kutoka shule mbalimbali za Halmashauri hiyo kwenda kusoma Ifinga na wanafunzi wa Ifinga kubadilisha mazingira kusoma maeneo mengine.
“Shule ya Sekondari Ifinga inajumla ya wanafunzi 73 ikiwa wanafunzi hao wanamaliza shule ya Msingi na kujiunga na Shule ya Sekondari katika kijiji hicho”.
Hata hivyo kwa upande wake Afisa Elimu Maalumu Tedy Sanga amesema Serikali imeleta fedha kiasi cha shilingi Milioni 128 kwaajili ya ujenzi wa Bweni katika Shule ya Msingi Madaba kwaajili ya wanafunzi maalumu.
Sanga amesema bweni hilo litasaidia wanafunzi maalumu kutoka maeneo mbalimbali ya Halmashauri kuishi na kusoma katika mazingira rafiki.
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Madaba
Septemba 13,2023.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa