SERIKALI imeleta shilingi Milioni 114 kwaajili ya ujenzi wa nyumba ya Mwalimu katika Shule ya Sekondari Wino Halmashauri ya Madaba.
Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri hiyo Sajidu Idrisa Mohamed ametembelea na kukagua mradi huo uliofikia hatua ya ukamilishaji amewapongeza walimu kwa usimamiaji mzuri wa ujenzi huo ambao utasaidia kuwa na makazi bora kwa Walimu wa Shule hiyo.
Hata hivyo Mohamed amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Rais Samia Sulluhu Hassan kwa kuleta fedha kwaajili ya ujenzi wa Nyumba za Walimu ambazo zitaleta Hamasa kwa Walimu.
“Nimshukuru Rais Samia kwa kutuletea fedha kwaajili ya ujenzi wa Nyumba za Walimu na Miradi mingine,pia niwapongeze walimu kwa usimamzi mzuri wa Nyumba hii “.
Kwa upande wake Mwalimu wa Shule ya Sekondari Wino Hassan Hussen amemshukuru Rais wa Awamu ya Sita kwa kuwapekea hela ya ujenzi wa Nyumba ya Mwalimu.
“Tunamshukuru kupitia ujenzi huu hata akija Mwalimu kutoka Massaki atajiona kama yupo Mjini kupitia ujenzi wa Nyumba hii Nzuri,na ukikaa katika nyumba hii lazima Mwalimu atajituma sana katika ufundishaji”.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
Mei 23,2023.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa