BARAZA la Madiwani Halmashauri ya Madaba limepitisha mpango wa bajeti ya matengenezo ya Barabara mwaka wa fedha 2023/2024 zaidi ya bilioni 2.
Kaimu Meneja Wakala wa Barabara za Vijijini (TARURA) Wilaya ya Songea Godfrey Mngale akisoma taarifa katika kikao cha Baraza la Madiwani amesema bajeti ya Mwaka 2022/2023 imetekelezwa na inaendelea kutekelezwa ikiwa mtandao wa barabara wenye jumla ya kilomita 629.7 ,kati ya hizo kilomita 196.31 za mjazo na 399.28 , za mkusanyo pamoja na 34.11 ni za jamii.
Mngale amesema hali ya Barabara katika Halmashauri hiyo kilomita 63 ambazo ni asilimia 10 ya barabara zina hali nzuri na kilomita 313 ambazo ni sawa na asilimia 49.7 zinahali ya kuridhisha na 253.7 zinahali mbaya ambazo sawa na asilimia 40.28
Hata hivyo amesema katika Halmashauri ya Madaba imegawanyika katika makundi manne ambapo kilomita 38.870 ni barabara za changarawe,kilomita 5.55 ni barabara za lami na zege na kilomita 585.275 ni barabara za udongo.
“Katika mwaka wa fedha 2022/2023 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba ilitengewa zaidi ya milioni 2 kwaajili ya matengenezo ya mtandao wa barabara kutoka vyanzo vikuu vitatu”.
Mngale amesema Mfuko wa Barabara uliidhinisha jumla ya shilingi milioni 638,mfuko mkuu wa Serikali kila jimbo la uchaguzi milioni 500, Serikali kupitia fedha za tozo bilioni moja.
“ Hadi kufikia Januari 2023 TARURA imepokea kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 815 ambazo ni sawa na asilimia 37.46 ya bajeti”
Mhandisi amesema katika utekelezaji wa bajeti ya mwaka wa fedha 2022/2023 Halmashauri ya Madaba imetekeleza jumla ya miradi 5 ikiwa na kilomita 24.81 zimefanyiwa matengenezo ya kawaida,kilomita 18.41 matengenezo katika maeeneo korofi,kilomita 7.37 matengenezo ya muda maalumu na makalavati 13 yametengenezwa kupitia mfuko wa jimbo.
Amesema jumla ya madaraja madogo 7 yanaendelea kujengwa kupitia fedha za tozo na jimbo la uchaguzi pamoja na ufunguzi wa barabara kilomita 53.12 kupitia fedha ya tozo ya mafuta hali ya matengenezo ya barabara Halmashauri ya madaba imefikia asilimia 52.16.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka kitengo cha Mawasiliano Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Madaba
Februari,13,2023.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa