MWENYEKITI wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Songea Thomas Masolwa amekuwa wa Kwanza kupata huduma katika Zahanati ya Mahanje iliyoanza kutoa huduma Novemba 22,2023 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.
Akizungumza mara baada ya kukagua Zahanati hiyo na huduma mbalimbali zinazotolewa katika Zahanati hiyo amempongeza Rais Samia kwa kutoa fedha Milioni 100 kwa awamu mbili kwaajili ya ujenzi wa Zahanati hiyo
“Rais Samia amewaona ameleta fedha Zahanati imekamilika na amewapunguzia wananchi kutembea umbali mrefu wa kwenda kutafuta huduma ya Afya”.
Hata hivyo Mwenyekiti ametoa rai kwa wananchi wa Kata ya Mahanje kuwapokea waganga wa 3 walioletwa na Serikali na kuwalea kama walivyokuwa mikononi mwa wazazi wao.
“Kwa niaba ya wazee wengine naomba muwapokee hao ni watoto wenu shida zao ziwe zenu wazazi wao wamewatunza vizuri leo wamekuja kuwahudumia ninyi usiku na mchana hivyo muwaone kama watoto wenu”.
Hata hivyo Mwenyekiti katika zoezi hilo amegawa vyandarua vya kuzuia maralia kwa wazee na wajawazito ikiwa huduma hiyo itaendelea kutolewa katika Zahanati hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Sajidu Idrisa Mohamed amesema Zahanati hiyo ilianza kujengwa kwa nguzu za wananchi kwa kutoa shilingi Milioni 10,Halmashauri ilitoa shilingi Milioni 19 ya mapato ya ndani na Serikali imetoa Milioni 100 kwa awamu mbili.
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Madaba
Novemba 22,2023.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa