WINO SACCOS wamefanya Mkutano mkuu na kupitisha bajeti ya mwaka wa Fedha 2023/2024 ya shilingi Milioni 191 na matumizi ya shilingi Milioni 181 na ziada ya milioni 10 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.
Akizungumza katika mkutano huo Mhasibu wa Wino SACCOS Agustino Wella amesema mwaka 2022 walipitisha bajeti ya mapato na matumizi shilingi Milioni 179 na matumizi ya shilingi Milioni 170 na mpaka kufikia sasa wametumia shilingi Milioni 124.
Hata hivyo Wella amesema WINO SACCOS imeanzishwa mwaka 1992 na leo umefanyika mkutano mkuu wa 30 na wamefanya uchaguzi wa viongozi watakao ongoza chama kwa mda wa miaka mitatu wakiwemo wajumbe wa bodi,kamati ya usimamizi mjumbe mwakilishi.
Kwa upande wake Afisa ushirika wa Halmashauri ya Wilaya ya Madaba Sadam fupi mara baada ya kusimamaia zoezi la uchaguzi wa viongozi wa chama hicho amesema viongozi wa Wino SACCOS waliochaguliwa wakasimie chama hicho kwa uadilifu.
“Tunategemea tukikaa kikao cha mwaka 2024 tukute mtaji wa chama umeongezeka mmekuta mtaji wa zaidi ya shilingi bilioni 1”.
Afisa Ushirika ametoa rai kwa viongozi waliochaguliwa kuhakikisha wanakuwa waaminifu ikiwa wanancha wamewachagua kwa kuwaamini na kuhakikisha mwaka 2024 mtaji wa chama unaongezeka,wakopaji wanaongezeka,wadaiwa sugu wamepungua na mstakabali wa chama ukiendelea mbele.
“Endapo mipango itaenda tofauti hatutasita kuwa chukulia hatua ikiwa wanachama wamewaamini na wamewachagu wameona mnafaa kusimamia watendaji wa wino SACCOS”.
Hata hivyoFupi amewapongeza Viongozi hao na kutoa rai wakatekeleze na kusimamia chama kanuni,sera za chama hicho kwa kuweka hisa,akiba na kulipa mikopo kwa wakati.
Kutoka kitengo cha Mawasilino Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
OKtoba 31,2023.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa