MAADHIMISHO ya siku Mbolea Duniani yamefanyika kwa siku tatu katika uwanja wa Majimaji mjini Songea mkoani Ruvuma.
Maadhimisho hayo yalizinduliwa na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Brigedia Jenerali Wilberth IbugeOktoba 11 na kufungwa na Waziri wa Kilimo Profesa Adolf Mkenda.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Brigedia Jenerali Wiberth Ibuge akitoa salamu katika Maadhimisho hayo amesema juhudi za kisera kwenye kilimo zimesababisha Mkoa wa Ruvuma kuongoza kwa kuzalisha mazao ya chakula kwa miaka mitatu mfululizo.
RC Ibuge amelitaja suala la upatikanaji wa Mbolea katika kilimo umeongezea tija na ufanisi wa uzalishaji wa Mazao hayo.
Hata hivyo amesema kwa mwaka huu bei ya mbolea imepanda kutokana na kutegemea viwanda vya nje ya nchi hali ambayo inaleta changamoto kwa wakulima.
“Kilio chetu wanaruvuma na Watanzania wote tunatambua siyo serikali imesababisha bei ipande bali uzalishaji wa Mbolea tunategemea viwanda vya nje na Corona ilipo tupiga wazalishaji walifunga viwanda na walipofungua kila mtu Duniani anataka Mbolea bila shaka lazima bei ipande’’,alisema RC Ibuge.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Udhibiti Mbolea Tanzania TFRA Profesa Antony Mshandete amesema idadi ya watu inatarajiwa kufikia bilioni 9.7 kufikia mwaka 2050 ambayo itasaidia kuongezeka uchumi wa viwanda na uhitaji wa kuzalisha mazao mengi kutoka katika eneo dogo.
Profesa Mshandete ameitaja kauli mbiu ya maadhimisho ya siku ya mbolea kwa mwaka 2021 kuwa ni Tumia Mbolea Bora kwa Tija na Kilimo Endelevu,ambapo amesema jukumu kuu ya TFRA kupitia kaulimbiu hiyo ni kusimamia ubora wa Mbolea.
Hata hivyo amesema katika kutekeleza kauli mbiu hiyo TFRA imekuwa na mafanikio mengi na kuendelea kuimarisha mifumo ya udhibiti wa Mbolea ili kuhakikisha wakulima wanapata Mbolea Bora kwa wakati wote.
“Mwaka 2016 hadi Septemba 2021 jumla ya mbolea zilizosajiliwa zilikuwa 356,Matumizi ya Mbolea yameongezeka uzalishaji mwaka 2015/2016 matumizi ya mbolea yalikuwa tani 296,036 na mwaka 2020/2021 matumizi ya mbolea yalikuwa 475,870”,alisema .
Hata hivyo Profesa Mshandete ameyataja mafanikio ya TFRA kuwa ni kuendelea kuimarisha mifumo ya udhibiti wa Mbolea ili kuhakikisha wakulima wanapata Mbolea bora,kuimarisha mfumo wa utoaji wa huduma za Mbolea ambapo hivi sasa huduma hutolewa kwa njia ya Mtandao.
Amezitaja changamoto za TFRA kuwa ni gharama za upatikanaji wa malighafi za kutengenezea Urea,Matumizi madogo ya Mbolea, Huduma isiyotoshelevu ya ugani,bei kubwa za Mbolea hasa katika soko la Kimataifa na Mabadiliko ya tabia ya Nchi ambayo yanayumbisha kwa Masoko.
Habari imeandikwa na Mwandishi wetu
Ruvuma
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa