WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji Profesa Kitila Mkumbo ametembelea eneo la uwekezaji wa Mbegu shamba la Silver land Ndolela lenye Hekta 5000 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.
Akizungumza mara baada ya kukagua eneo hilo amesema wawekezaji hao wanazalisha mbegu za aina nne ikiwemo Maharage,Viazi,Ngano na Mahindi.
Mkumbo amesema katika Nchi ya Tanzania moja ya changamoto ya Kilimo ni mbegu ambazo zinatumiwa kwa mda mrefu na kupelekea kulima eneo kubwa na kuvuna kidogo hivyo uwepo wa wawekezaji hao utapelekea kutatua changamoto uhaba wa Mbegu.
“Mara nyingi Waziri wa Kilimo amesema changamoto za Kilimo ni swala la Mbegu na Mbolea hayo ni maeneo makubwa yanayosumbua uwepo wa wawekezaji hao ni msaada mkubwa ambao wamewekeza katika Halmashauri ya Madaba”.
Hata hivyo Mkumbo amepokea changamoto wanayokutananayo wawekezaji hao ikiwemo swala la chokaa ambayo wanaagiza kutoka Mkoa wa Tanga kwaajili ya kuchanganya kwenye ardhi ya Ruvuma kwasababu ina acidi.
Amesema Wilaya ya Songea ina chokaa watahakikisha Serikali inatafuta wawekezaji kwaajili ya kuchakata chokaa ili wananchi wa Ruvuma waweze kutumia Chokaa inayopatikana ndani ya Mkoa na itawasaidia kupunguza gharama za matumizi makubwa ya Mbolea
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Songea Wilman Ndile katika ziara hiyo amesema Waziri Kitila Mkumbo amejionea uwekezaji huo ikiwa wawekezaji wengi kuwekeza katika viwanda na kukwepa kuwekeza kwenye kilimo.
Amesema Wawekezaji wa Silver land Ndolela wameamua kuwekeza katika kilimo ikiwa Wilaya ya Songea kuna wawekezaji wawili akiwemo Avivu amewekeza katika kilimo cha Kahawa na Silver Land Ndolela amewekeza katika Mazao ya chakula.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
Agosti 23,2023.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa