WATUMISHI wanaotarajia kustaafu Halmashauri ya Wilaya ya Madaba wamepewa semina ya kujua mafao yao mara baada ya kustaafu.
Semina hiyo imetolewa na Afisa Mwandamizi kutoka mfuko wa hifadhi ya jamii kitengo cha huduma Mkoa wa Ruvuma (PSSSF) Jimy Tanasho amesema ili mtaafu ajue kile alichochangia na anachostahili pindi anapokuwa kwenye utumishi na hata anapokuwa amestaafu.
“ Lengo Mtanzania ajue haki yake baada ya maisha ya kazi kukoma”.
Tanasho amesema lengo la Semina hiyo imetolewa ili kuondoa kelele nyingi kwa wastaafu mara nyingi kudai kwamba mafao yao yamepunjwa.
Amesema mafao ya mtumishi mwanamke ya uzazi yanapatikana kuanzia mtoto wa kwanza hadi wanne ambapo anastahili mara baada ya kuchangia miaka mitatu na kuendele.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
Julai 25,2024
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa