WATUMISHI Halmashauri ya Wilaya ya Madaba wanaoishi kilomita 7 kutoka makazi yalipo hadi Ofisi ya Halmashauri kutozwa kiasi cha shilingi 4,000/= kwa siku.
Watumishi hao wameiomba Serikali kuingilia kati swala hilo la nauli za Bajaji na Bodaboda mbele ya Mbunge Viti maalumu anayewakilisha Watumishi Tanzania Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala bora Alice Kaijage alipo zungumza na Watumishi hao katika ukumbi wa ofisi ya Mkurugenzi.
Kaijage aliposikiliza kero hiyo ametoa rai kwa viongozi wa LATRA kushughulikia jambo hilo ambalo linapelekea watumishi hao kutoa kiasi kikubwa cha nauli kwa siku ambacho siyo halali kulingana na umbali wa eneo hilo.
Kwa upande wake Katibu wa chama cha wafanyakazi Mashambani na Kilimo Tanzania Ahimidiwe Pallanngyo amesema viongo wa LATRA wahakikishe wanalifanyia kazi swala hilo ikiwa Bodaboda na Bajaji wanajipangia nauli wenyewe wanavyoweza.
“Mimi nimepigwa sana nikija Madaba nikifika Songea nitaenda Ofisi za LATRA nitawaambia ili haki itendeke”.
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
Novemba 16,2023.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa