WATUMISHI wa Halmashauri ya Wilaya ya Madaba Mkoa wa Ruvuma wamepewa mafunzo ya kodi ya zuio katika mfumo ulioboreshwa wa mamlaka.
Mafunzo hayo yametolewa na Mhasibu wa Mamlaka ya Mapato (TRA) Mkoa wa Ruvuma Amimo Ndaro amesema mafunzo hayo yamelenga makusanyo yanayofanywa na watumishi waliopo katika Halmashauri kuto wasilisha kwa Kamishna wa kodi za ndani pamoja na kuto jua na kupata oda fomu (Conrol number) ili waweze kuwasilisha katika kodi za ndani
“Tukaona tupite kwenye Halmashauri na kuelimisha watumishi wapo wanaojua wengine hawajui wengine wafanyakazi wapya wanafanya kazi zinazohusiana na uhasibu wapo waliokumbushwa na wengine wamepata elimu kwa mara ya kwanza”
Hatahivyo ndaro amesema kupitia mafunzo hayo kumekuwa na mwitikio ikiwa baadhi ya washiriki ni mara yao ya kwanza wamejifunza na kupata pakuanzia na baada ya mafunzo haya kodi iliyo nyingi itawasilishwa kwa kamishna wa kodi za ndani.
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
Februari,20,2024.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa