WATUMISHI Halmashauri ya Wilaya ya Madaba wemejitokeza kupata kinga tiba ya Usubi wakiongozwa na kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Maternus Ndumbaro ambae ni Mkuu wa Idara ya Elimu Sekondari.
Zoezi hilo limefanyika Katikan ukumbi wa Halmashauri na wemepewa Elimu ya ugonjwa huo unaoathiri ngozi na macho na kusababishwa na minyoo iitwayo (Onchocerca Volvulus).
Mratibu wa Magonjwa yasiyopewa kipaumbele Halmashauri ya Madaba Dokta Betty Mbawala amesema Minyoo hiyo huenezwa na inzi weusi wadogo wanaozaliana kandokando ya mito yenye maji yanayoenda kwa kasi.
Mratibu wa Magonjwa hayo amezitaja dalili za ugonjwa huo ikiwemo maambukizi ya vimelea vya usubi vinavyosababisha na kuwasha kwa ngozi,ukurutu usiotibika,kuwa mithili ya ngozi ya kenge au Mamba,kuwa na vinundu sehemu ya mifupa pamoja na kuwa na ngozi yenye mabaka mithili ya mtu aliyeungua na moto au kama ngozi ya chui.
Hata hivyo Mratibu amewakumbusha wananchi mara wanapoona dalili hizo wawahi kituo cha kutolea huduma za Afya kwa uchunguzi na matibabu zaidi.
Mbawala ameyasema madhara yanayoweza kutokana na ugonjwa wa Usubi ikiwa pamoja na ngozi kuharibika, kutoana vizuri na kupelekea upofu wa macho, kushindwa kufanya kazi kupelekea umaskini na utegemezi katika Familia.
“Ugonjwa wa Usubi unazuilika kwa kumeza kinga tiba kwa kila mtu kuanzia umri wa miaka mitano kila zinapotolewa kwenye jamii”.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
Agosti 22,2023.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa