HALMASHAURI ya Wilaya ya Madaba imeanza zoezi la ugawaji wa dawa za magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele ukiwemo ugonjwa wa usubi (Vilera).
Zoezi hilo limeanza katika maeneo mbalimbali ya halmashauri hiyo wataalam wa afya wamegawa dawa hizo kwa wafanyakazi wa kampuni ya Slver land Ndolela jumla ya watumishi 235 wamepata kinga tiba.
Ugonjwa wa Usubi husababishwa na minyoo inayoenezwa na inzi weusi wadogo wanaokaa kando ya mito yenye maji yaendayo kasi na kupelekea ngozi kuwasha au kuwa na mabaka mabaka mithili ya mamba au mjusi na kupelekea upofu kwa binadamu.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka kitengo cha mawasiliano halmashauri ya Wilaya ya Madaba
Septemba 3,2024.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa