Shirika lisilo la Kiserikali Standing Order Voice wametoa Elimu ya kujikinga na saratani ya ngozi kwa watu wenye ulemavu wa ngozi (Ualbino) Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
Elimu hiyo imeambatana na kupimwa Afya zao na kupewa matibabu Madaktari wa shirika hilo wamewaasa maalbino kuvaa nguo zinazoficha mwili, kofia zenye uwigo mpana pamoja na kupaka mafuta wakati wa asubuhi na mchana.
Huduma hiyo imetolewa katika Kituo cha Afya Madaba Madaktari wametoa rai kwa maalbino kuwa wasafi ili waweze kuwa mrembo kama watu wengine
“Mtu ukiwa Albino haikuzii kuto kuwa mrembo kama watu wengine zingatieni usafi pamoja na kuvaa vizuri”.
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Halmshauri ya Madaba
Januari 24,2024
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa