KATIBU Tawala msaidizi Uzalishaji na Uchumi Mkoa wa Ruvuma Jeremia Sendoro amefungua mafunzo ya uandaaji wa vitabu na Mbinu za kupata hati safi kwa wahasibu na waandishi wa AMCOS kanda ya Kusini.
Akizungumza katika ufunguzi wa Mafunzo hayo amesema Mafunzo ya wahasibu na waandishi wa vyama vya Ushirika wa Mazao na Masoko (AMCOS) yamejumuisha mikoa ya Lindindi,Mtwara, Ruvuma na Mbeya na kufanyika katika ukumbi wa SUT SACCOS Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma.
“Elimu na Mafunzo ni moja kati ya Misingi saba ya Ushirika ya Kimataifa, hivyo mafunzo ni utekelezaji wa msingi katika kuimarisha vyama vya ushirika kwa lengo la kuvifanya vyama kuwa na hati safi “.
Sendoro amesema Ushirika utakuwa na maana kwa Taifa ikiwa utaongeza uzalishaji na kurahisisha masoko ya Uhakika ya mazao,na hatimaye kushinda vita dhidi ya umaskini.
“Naomba niwakumbusheni kuwa ushirika ni dhana muhimu ya kujenga uchumi imara na wenye nguvu katika kupunguza na kama si kuondokana kabisa na mfumo wa ushirika ni mfumo pekee na muhimu wa kupambana na vita dhidi ya uchumi”.
Sendoro amesema Serikali inatambua,Ushirika ni dhana pekee ya kumkomboa mkulima na mnyonge kiuchumi ,Ushirika umeelekezwa katika ilani ya utekelezaji wa chama cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2020 hadi 2025 kuwa ni nyenzo muhimu ya kukuza Uchumi.
Katibu Tawala msaidizi ametoa wito kwa viongozi na watendaji wa vyama vya Ushirika kuwa karibu na wakulima wakati wote wa shughuli za msimu ili kubaini na kutatua changamoto mbalimbali za utekelezaji wa shughuli za masoko,kusimamia na kuhakikisha wakulima wote wanauza mazao kupitia mifumo iliyoelekezwa na Serikali.
Kwa upande wake Afisa mipango Emmanuel Danda amesema kuwa changamoto zinazosababisha wanachama kupata hati chafu ni elimu katika eneo la uhasibu kupelekea kuwa na hati chafu kwa vyama vya ushirika.
Danda amesema kwa msimu huu na ujao wamejipanga kwa kutafuta wadau ili waweze kuimarisha masoko na kuwajengea uwezo watendaji ili mifumo ya vyama vya ushirika iweze kufanya vizuri kwa wakulima.
Mwenyekiti wa Mafunzo hayo Hamza Rashi Mbutuka akisoma Risala kwa mgeni rasmi amewapongeza waandaji wa mafunzo ambao ni wakufunzi kutoka chuo cha Ushirika Moshi,Chuo cha uhasibu na maafisa ushirika kutoka Wilaya mbalimbali zilizomo ndani ya Mkoa na nje ya Mkoa.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka ofisi ya Habari Mkoa wa Ruvuma
Septemba 21,2021.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa