MSIMAMIZI wa Uchaguzi Jimbo la Madaba Sajidu Idrisa Mohamed amefungua mafunzo ya siku mbili kwa Wasimamizi wakuu na wasaidizi ya uchaguzi Mdogo wa Udiwani Kata ya Mtyangimbole.
Akizungumza na wasimamizi hao amesema jumla ya Wasimamizi 62 wakiwemo 20 Wasimamaizi wakuu na wasaidizi 40 2wawili ni wa akiba wanaofanyiwa mafunzo ya uchaguzi mdogo wa Udiwani Kata ya Mtyangimbole .
Amesema Mafunzo hayo ya siku Mbili kwa wasimamizi wa Uchaguzi yanalenga kutoa maelekezo namna Wasimamizi wakuu na wasaidizi wanavyotakiwa kutekeleza majukumu yao kwa mujibu wa sheria,taratibu na kanuni za uchaguzi sura namba 343.
“Mmeteuliwa kufanya hii kazi kwa kuzingatia weledi na uaminifu hivyo sitegemei miongoni mwenu kwenda kinyume na maelekezo mtakayopewa”.
Msimamizi wa uchaguzi Jimbo la Madaba amesema kuwa wasimamizi hao wamekula kiapo cha kutunza siri na kujitoa uanachama wa chama cha siasa na kuzingatia taratibu na kanuni ,taratibu za uchaguzi.
“Narajia kwa mda wote wa mafunzo mtakuwa makini wasikivu katika kuhakikisha mnaelewa maelekezo mnayopewa na wasimamizi wasaidizi wa Jimbo ili mkatekeleze vema majukumu yenu”.
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Madaba
Septemba 16,2023.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa